Changu Chako, Chako Changu

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 7:40:59
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

Episódios

  • Utamaduni wa ndoa kabila la wamakonde na wahangaza kutoka nchini Tanzania sehemu ya 2

    29/09/2024 Duração: 20min

    karibu, Jumapili nyingine kuwa nami katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia na utamaduni wa mambo mbalimbali, le Parler francophone na Muziki. Wiki iliopita nilikuletea Utamaduni wa ndoa kutoka makabila ya Wamakonde na wahangaza, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili. Na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba za shughuli za kitamaduni kutoka Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam, Tutamaliza na Wimbo wa Ibrah kutokz Tanzania

  • Utamaduni wa watu wa makabila ya wahangaza na wamakonde kutoka nchini Tanzania

    22/09/2024 Duração: 20min

    Katika makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Amua Rushita kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na Hillary Alexanda Ruhundwa kutoka Mkoa wa Ngara nchini Tanzania kuzungumzia utamaduni wa ndoa kulingana na makabila hayo mawili. Kumbuka pia nawe unaweza kushiriki moja kwa moja studio au kwa njia ya simu. Wasiliana na mtangazaji wako asiependa makuu kufahamu zaidi.

  • Toleo la 11 la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon kutolewa huko Benin

    26/08/2024 Duração: 19min

    RFI inaandaa toleo la kumi na moja la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kwa heshima kwa waandishi wake wawili waliouawa kaskazini mwa Mali  Novemba 2, 2013. Bourse hii, ambayo huwafunza waandishi wa habari vijana kumi wa redio na mafundi vijana kumi wa kuripoti kila mwaka, iko wazi. kwa wagombea kutoka nchi zote za Afrika zinazozungumza Kifaransa. Mafunzo hayo yatafanyika Cotonou. Maombi yamefunguliwa hadi Jumapili Agosti 25 saa sita usiku saa za Paris.

  • Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa mahari kwa baadhi ya makabila barani Afrika

    26/08/2024 Duração: 19min

    Makala haya yanaangazia kuhusu gharama ya sherehe za harusi katika karne hii, hususan ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kufanaikisha sherehe.

  • Changu chako chako changu Tasnia ya ulimbwende sehemu ya pili

    13/08/2024 Duração: 20min

    Karibu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu Ulimbwende au Model,

  • Changu Chako Chako Changu tasnia ya ulimbwende sehemu ya kwanza Agost 04 2024

    04/08/2024 Duração: 20min

    Karibu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea mambo mbalimbali ya utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sanaa ya Ulimbwende au Model, na kwenye la parler francophone nitakuletea shughuli zinazoendelea kwenye vituo vya Alliance francaise za ukanda kipindi hiki cha michuano ya Olympiki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue.

  • Historia ya kabila la Wabukusu pamoja na sanaa ya muziki kutokea kwa Bendi ya An Noor

    21/07/2024 Duração: 20min

    Karibu kwenye makala ya  changu  chako ,chako  changu juma hili ukiwa nami Florence Kiwuwa. Na kwenye kipengele cha historia hii leo tutaangazia historia ya kabila la Waluhya wanaofahamika kama wabukusu kisha kwenye kipengele chetu cha pili cha LeParle Francophone tutaangazia maonyesho ya Taarab yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance France kisha tutamalizia na mwanamuziki wa Kenya almarufu kama Freshely Mwamburi.

  • Matumizi ya lugha ya kiswahili katika enzi ya Kijiditali

    16/07/2024 Duração: 20min

    Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 afrika mashariki na kwenye makala haya ya changu chako,chako changu ,Florence Kiwuwa amefanya majadiliano na wanafunzi katika chuo kikuu cha Multmedia ili kujua kuhusu mchango wa lugha hii katika kuendeleza utamaduni na utengamano na vilevile katika kipengele cha muziki amemuangazia mwanamuziki wa Tanzania Harmonize.

  • Changu Chako Chako Changu maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 14 ya RFI Kiswahili

    07/07/2024 Duração: 19min

    Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu jumapili ya leo ambapo nakulrtea Makala maalum kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu Ple RFI Kiswahili ilipoanza kupeperusha matangazo yake mubashara kutoka nchini Tanzania ambapo ilikuwa idhaa ya kwanza ya Kimataifa kutangaza ikiwa Afrika mashariki. Na kwenye Muziki nitakuletea Burudani ya Muziki wa Idd Aziz Kiswahili kitukuzwe wakati huu tukielekea kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani. Mimi naitwa Ali Bilali, Bienvenue ama Karibu.  Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa @billy_bilali

  • Changu Chako Chako Changu, maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa DRC

    06/07/2024 Duração: 20min

    Makala haya Ali Bilali anazungumzia kuhsu maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa DRC.

  • CHANGU CHAKO CHAKO CHANGU HISTORIA NA UTAMADUNI WA WATU WA KABILA LA WANUBI

    16/06/2024 Duração: 20min

    Eid Mubaraka kwako mskilizaji wa RFI Kiswahili popopte pale ulipo ausubuhi hii. Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu. Leo nakuletea Historia ya watu wa Kabila la Wanubi, na kwenye Muziki nakupeleka  nchini Burundi ambapo nazungumza na msanii wa kizazi kipya, Keypeacvaldiny. mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu Karibu ama bienvenue. Jina lake halisi ni Nzeyimana touré hamissi, anatumia jina la kisanii a @keypeac_valdyn amezaliwa April 8 mwaka 2002 jijini Bujumbura inchini burundiAlianza muziki mwaka 2017, ila sababu ya harakati za masomo na familia alilazimika kuachana kabisa na muziki na kujikita zaidi na masomo. Baada ya kumaliza shule mwaka 2023 akaamuwa kurejea kwenye tasnia ya Muziki ambapo amekuja na EP yake iliowekwa hewani tangu April 15 mwaka 2024. EP yake hiyo ina nyimbo 3 ambazo ni:Track n°1.carolinaTrack n°2.sorryTrack n°3.mmmhna songs hizo zote zipo kwenye platforms zake zote anapatikana kwa jina la @keypeac valdynyupo kwenye platforms  zifwatazo kama : a

  • Historia ya madaraka Day nchini Kenya na ziara ya Mistachampagne studio za RFI Kiswahili

    04/06/2024 Duração: 20min

    Karibu katika makala ya leo changu chako chako changu ambapo leo nakuletea historia ya siku ya madaraka ambayo huadhimishwa kila Juni Mosi nchini Kenya. Na kwenye le parler francophone kama kawaida nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise za ukanda. Na Kwenye Muziki nitakuwa naye Mr Champagne msanii kutoka nchini Burundi ambaye yupo nchini Kenya kwa ajili ya kutangaza wimbo wake mpya Niko tu. Mimi ni Ali Bilali bienvenue ama karibu. Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali 

  • Historia na utamaduni wa kabila la wanyakyusa sehemu ya pili

    30/05/2024 Duração: 20min

     Karibu katika Makala haya changu chako chako changu, jumapili ya leo ambapo nakuletea awamu ya pili ya makala kuhusu historia na utamaduni wa watu wa kabila la Wanyakyusa, na kwenye Muziki nakupa muendelezo wa mazungumzo na wasanii Kidum Kibidon na EstherNish. Mimi ni Ali Bilali. Bienvenue.

  • Historia na Utamaduni wa wanyakyusa na muziki wa Kidum pamoja na Esther Nish

    19/05/2024 Duração: 20min

    Furaha ilioje kukutana nawe Jumapili ya leo katika Makala Changu chako Chako Changu, ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophpone na Muziki ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya makala kuhusu historia ya Wanyakyusa, na kwenye Miuziki nitakuletea mwanamuziki Esthernish pamoja ni Kidum. Mimi ni Ali Bilali bienvenue. Ama Karibu. Kumbuka pia kutufollow kwa Instagram @billy 

  • Sehemu ya makala kuhusu utamaduni wa waluo na waluhya hasa kwenye maswala ya ndoa

    16/05/2024 Duração: 20min

    Karibu katika Makala haya changu chako chzako changu Jumapili ya leo ambapo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu tamaduni za wa Luhya na wa luo nchini Kenya ambapo sasa tutaangazia kuhusu tamadunbi za ndoa, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na kwenye muziki nitakuletea mwanamuziki Mbosso kutoka nchini Tanzania. Mimi ni Ali Bilali Karibu.

  • Utamaduni wa watu wa kabila la Waluo na Waluhya kutoka nchini Kenya

    05/05/2024 Duração: 20min
  • Maoni ya washiriki katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani sehemu ya mwisho

    21/04/2024 Duração: 20min

    Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, na leo tunahitimisha mlolongo wa Makala kuhusu kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika huko Mbeya, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni kutoka Alliance Francaise ya Arusha na Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki King Kaka kutoka nchini Kenya.

  • Sehemu ya tatu ya Makala kuhusu kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani

    14/04/2024 Duração: 20min

    Ni Jumapili nyingine tunakutana katika Makala Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler francophone na Muziki, leo ninakuletea mazungumzo kuhusu ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili, ikiwa ni kauli mbiu ya kongamano la nne za idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika mkoani Mbeya Mwezi Machi. Na kwenye le parler francophone nitakuletea mradi wa Creation Afrika unaonadaliwa na Allliance francaise ya Nairobi

  • Kongamano la idhaa za kiswahili duniani, umuhimu wa kujifunza lugha ya Kiswahili

    09/04/2024 Duração: 19min

    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Msimamizi wa kituo cha radio China Kimataifa ambaye ni raia wa China kufahamu zaidi kwanini alivutiwa na swala la kujifunza lugha ya kiswahili, ni katika muktada wa kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika Mbeya nchini Tanzania. Kwenye Muziki utasikiliza wimbo wa mwanamuziki Lupman mwenye asili ya Burundi anaefanya kazi yake huko Sweeden. https://www.youtube.com/watch%3Fv%3DdsIZZ0MmadE

  • Kongamano la nne la idhaa za kiswahili duniani "Tasnia ya habari na ubidhaishaji Kiswahili duniani"

    31/03/2024 Duração: 20min

    Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambyo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo kuhusu Kongomano la nne la idhaa za Kiswahili duniani. Kwenye le Parler francophone nitakueleza ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Idd Aziz kutoka nchini Kenya.

página 1 de 2