Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 3:59:19
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Episódios

  • Wataalam wa mazingira: Kuchakata plastiki sio suluhu ikiwa nchi zinazalisha zaidi

    10/12/2024 Duração: 10min

    Mkutano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki ulikamilika mwanzoni mwa Disemba 2024 bila mwafaka kufikiwa, wataalam wa mazingira wakisema pendekezo la kuchakata plastiki wakati nchi nyingine zikiendelea kuzalisha sio suluhu la tatizo hilo. Kwenye makala hii leo tunaangazia athari za plastiki kwa afya na mazingira, suluhu zinazopendekezwa lakini pia kupata ufafanuzi zaidi kilichokwamisha kupatikana kwa mkataba wa kumaliza tatizo linalosababishwa na uchafuzi wa plastiki.

  • COP29: Wanamazingira wapendekeza ufadhili zaidi kwa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

    19/11/2024 Duração: 09min

    Mkutano wa hali ya hewa COP29 ukiendelea nchini Azerbaijan, masuala yanayoibua changamoto ni ufadhili, mchakato wa kuondokana na mafuta kisukuku, athari ambazo zimekumba bara la Afrika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka kwa viwango vya joto lakini pia suluhu zinazopendekezwa na wataalam wa mazingira. Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye mkutano wa COP29 ni uwajibikaji wa ufadhili haswa kutoka mataifa tajiri ambao wanachangia kwa viwango vikubwa uchafuzi wa mazingira wakati athari zake zinaathiri nchi zisizojiweza na shirika la mazingira la Greenpeace Africa linapendekeza mustakabali wa nishati mbadala na haki ya hali ya hewa kwa Afrika.Kwa mengi zaidi bonyeza ili kusikiliza makala. 

  • Ripoti ya mazingira ya UNEP kuhusu pengo la uzalishaji wa gesi chafu duniani 2024

    31/10/2024 Duração: 10min
  • Jamii Pwani ya Kenya wapinga mradi wa nyuklia kutokana na athari kwa mazingira

    29/10/2024 Duração: 09min
  • DRC:Jamii ya mbilikimo wakemea uharibifu wa misitu unaofanywa na makundi ya waasi

    09/10/2024 Duração: 10min
  • Siku ya kimataifa ya uhamasisho kuhusu upotevu na utpaji wa chakula

    30/09/2024 Duração: 10min
  • Siku ya kimataifa ya kufanya usafi wa mazingira na matumlizi ya teknolojia

    23/09/2024 Duração: 10min

    Katika dunia ya sasa ambapo ukuaji wa teknolojia ni wa kasi ya juu, wabunifu katika jamii za pwani nchini Kenya, wamekumbatia matumizi ya teknolojia katika kupiga jeki juhudi za kupunguza taka kwenye mazingira wanayoishi.

  • Wahifadhi wahofia kudidimia kwa tembo aina ya "Super Tusker'

    06/09/2024 Duração: 09min

    Wanasayansi na wahifadhi wameibua hofu ya kutokomea kabisa kwa tembo aina ya "Super Tusker" ambaye pembe yake moja ina kilo takriban 45, ikiwa hatua hazitachukuliwa ili kuzuia uwindaji wao.Katika mbuga ya Amboseli inayopakana na Kenya na Tanzania, ndovu hawa wamebaki kumi pekee.

  • Mchango wa mashirika yasio ya kiserikali kuwezesha upatikanaji wa maji safi kwa jamii nchini Kenya

    06/09/2024 Duração: 10min

    Katika maadhimisho ya wiki ya maji duniani 2024, makala haya yameangazia mradi wa WASH unaofanywa na shirika la SHOFCO mtaani Kibera, kusambaza maji safi ya matumizi kwa wakaazi wa kitongoji hicho chenye changamoto za upatikanaji wa maji safi.

  • Matumizi ya taka za chupa za plastiki kuendeleza kilimo bila mchanga(Hydroponic farming)

    12/08/2024 Duração: 09min

    Kundi la vijana la Vision Bearers la mtaani Mathare, jijini Nairobi linavyotumia taka za chupa za plastiki kuendeleza kilimo bila mchanga(Hydroponic farming)

  • Kenya: Namna mabaki ya ngozi ya samaki yanavyotumiwa kuhifadhi mazingira

    05/08/2024 Duração: 09min

    Kwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.Hata hivyo wenyeji sasa wengi wao vijana wameanza kutumia taka hizo kutengeza bayogesi na bidhaa zingine kama vile viatu,nguo,begi mifuko na kadhalika hivyo kubuni ajira na kuinua uchumi. Katika fuo za Dunga kando na ziwa Victoria kaunti ya kisumu nchini Kenya,wafanyabiashara hapa wanatumia bayogesi kukaanga samaki na  kuwauzia wateja wanaotalii êneo hili.Bayogesi hii inayotengenezwa kutokana na mabaki ya samaki ,imewafaidi wenyeji wa hapa kupunguza gharama ya matumizi vile vile kutunza mazingira. Caroline Achieng ni mfanyabiashara wa samaki.“Tunadumisha usafi kwa sababu wageni wanakuja hapa lazima tudumishe usafi ndio mazingira yetu yasiharibike,mradi huo umesaidia sana kwa sababu wametusaidia kuchukuwa hizi takataka za samaki kama matumbo,wanatengeneza nayo bayogasi hivyo kupunguza uchafu”alisema  Caroline Achieng m

  • Uhifadhi wa mbegu za kitamaduni na sera zinazotishia mapato ya wakulima wadogo nchini Kenya

    29/07/2024 Duração: 10min
  • Uhifadhi wa mbegu za kitamaduni na kiasili na shirka la Seed Savers Network

    22/07/2024 Duração: 10min
  • Ugeuzaji wa taka za plastiki kuwa matofali maalum(Cabro) inayotumika kutengeneza barabara

    17/06/2024 Duração: 10min

    Juma hili katika makala ya mazingira leo dunia yako kesho, mwandishi wetu wa Goma Benjamin kasemabe, ametuandalia ripoti ya namna mjasiriamali Irene maroy anavyogeuza taka za plastiki kuwa matofali maalum maarufu kama Cabro inayotumika kutengeneza barabara.

  • Uboreshaji wa ardhi, kuimarisha ustahimilivu kwa ukame, na kupambana na kuenea kwa majangwa

    12/06/2024 Duração: 09min
  • Mradi wa Sola katika kisiwa cha Ndeda, nchini Kenya, waleta mabadiliko kwa wakaazi

    21/05/2024 Duração: 09min
  • Katika makala haya utafahamu kuhusu vimbunga na athari zitokanazo na vimbunga

    20/05/2024 Duração: 10min
  • Majadiliano kuhusu mkataba wa kisheria wa kimataifa kudhiti uchafuzi wa taka za plastiki

    14/05/2024 Duração: 10min
  • Nchi za Afrika Mashariki zaendelea kushuhudia mvua kubwa zikihusishwa na El Nino

    06/05/2024 Duração: 10min
  • Hali ya mafuriko katika nchi za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika

    29/04/2024 Duração: 10min

    Kulingana na jumuiya ya IGAD,  zaidi ya vifo 190 vimeriotiwa  katika eneo la pembe ya Afrika, huku watu wengine laki 7 wakiyahama makazi yao.

página 1 de 2