Habari Za Un

UNICEF yatoa mafunzo ya kutengeneza sodo kwa kijana mkimbizi wa dani nchini Sudan

Informações:

Sinopse

Sodo au taulo za kike, vile vile pedi,  ni muhimu kwa wanawake na  wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya  usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan. Msaada wa kifedha kutoka  Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, vilabu vya usafi vya UNICEF, na Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID,  vijana wakimbizi wa ndani wanawezeshwa kupata suluhisho kwa changamoto za usafi wanazokutana nazo, wakati wa vita na ukimbizi. Mmoja wa vijana hawa wakimbizi ni Samer mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye amefundishwa kutengeneza sodo na sasa, anazisambaza bure kwa wanawake na wasichana wakimbizi wa ndani katika jimbo la Atbara, nchini Sudan.Nikataka kujua jinsi Samer anatengeneza sodo hizo…"Nashona kati ya vipa